Mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewapa ushauri viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu hama hama ya baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho akiwataka wajipange na kujipima.

Ameyasema hayo mara baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kusema kuwa baadhi ya viongozi wao hata yeye wamekuwa wakipigiwa simu na kupewa ahadi nyingi nzuri ili waweze kuachia nafasi zao na kujiunga na CCM.

“La msingi ni kumjenga mwanachama wako kiitikadi hasa kwa kumjengea imani, Kama hana imani na chama atahama tu kwani hayo uliyoyasema akibaki kwenye chama chake atayapata tu. La msingi kuangalia je wanachama wana imani?! Kubwa zaidi ni kujipima je, mnasimamia misingi ya chama?”ameandika Kasesela kwenye ukurasa wake wa Twitte

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 18, 2017
Zuma awatahadharisha wafuasi wa ANC