Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema kimetoa msimamo wake juu ya baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakihama na kusema wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli

Mrema amesema kuwa viongozi hao wanapoondoka waseme sababu za kweli zinazowafanya kuondoka CHADEMA na kwenda CCM na si kuwadanganya wananchi kwa kutoa sababu zisizo na msingi ambazo ni uongo.

Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya ‘hapa kazi tu’ na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi,”amesema Mrema.

Aidha, Mrema amesema kuwa chama chao kipo imara na wataendelea na ajenda zao bila kuyumbishwa na wimbi la watu wachache ambao wamekuwa wakihama chama hicho kwa kutoa sababu nyepesi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wataendelea kujenga Taifa na Chama chao bila kujali njaa za baadhi ya watu wala maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama.

 

Video: Kama vyuma vimekaza wekeni grisi- JPM, Mwaka 2017 wapinzani wamevugwa
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 15, 2017