Mbunge wa Jimbo la SIHA lililopo mkoani Kilimanjaro, Godwin Mollel amejiuzulu nafasi ya ubunge wa jimbo hilo na kuomba kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

Mollel amesema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo mara baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli kwani walichokuwa wakipigania upinzani kwa sasa kinatekelezwa na rais.

“Baada ya kuwa mbunge wa upinzani kwa muda wa miaka miwili sasa, nimewatumikia watu wangu wa jimbo la SIHA, nimeshirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo, hivyo nimeamua kujiuzulu ubunge na uanachama wa Chadema, hivyo naomba kujiunga na CCM,”amesema Mollel

Hata hivyo, Mollel amesema kuwa ameamua kujiuzulu na kuomba kujiunga CCM ili aweze kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi.

Askari afariki dunia, atumbuliwa risasi ya kichwa
Atiwa mbaroni kwa kuuza watoto pacha