Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amegawa zaidi ya hati 80 za ardhi kwa Wananchi wa kijiji cha Wagana ikiwa ni lengo la kuwasaidia wananchi hasa wanawake waishio vijijini kuwa na matumizi bora ya ardhi.
Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa hati hizo kwa wanawake, Mh. Kasesela amewataka kuzitumia hati hizo katika kujikwamua kiuchumi ikiwamo kukopa fedha katika taasisi mbalimbali badala ya kuziweka ndani pekee.
Amesema wilaya ya Iringa itakua mfano wa kuigwa juu ya ugawaji wa hati za ardhi kwa wananchi ambapo mpala sasa zaidi ya vijiji 33 katika wilaya ya Iringa vimekamilisha mpango wa matumizi bora ya ardhi na wananchi wake wamekwisha patiwa hati hizo.
Aidha, Mh. Kasesela amesema lengo la Serikali ni kuwakwamua wananchi wake kufikia uchumi wa kati hivyo jamii inapaswa kuzingatia matumizi bora ya ardhi .
Hati hizo zimegawiwa kwa Wananchi kupitia kwa taasisi ya TARWOC yenye lengo la kuwawezesha wanawake kumiliki ardhi.