Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amethibitisha wagonjwa kulazimisha kuondokoka katika hospitali ya rufaa Amana na kutaka kurejea nyumbani kwa madai kuwa huduma zinatolewa hadhiridhishi.
Mjema amesema kuwa kama kuna mtu ameondoka watampata kwani wagonjwa wote waliochukuliwa wanajulikana nyumba zao, hivyo watawafuatilia ili wasisambaze ugonjwa huo.
“Hao wagonjwa walikuwa wanatishia kuondoka, kuhusu watu kutoroka na kupanda daladala hilo bado sijalijua nitafuatilia kujua ni watu wangapi waliondoka,” amesema Mjema
Mkuu huyo wa wilaya amesema kwa wale ambao wamepata nafuu wasubiri kupewa maelekezo ya wataalamu, kutoroka haitasaidia kwani huko mtaani wakirudi watakimbiwa.
Hayo yamejiri baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kunawagonjwa wa homa kali ya mapafu (covid 19) ambao walikuwa wakipatiwa matibabu hospitali ya Amana wametoroka jana usiku.