Bastola aina ya T0620-14J0077 iliyoibiwa kwa mfanyabiashara mjini Kahama, ikiwa na risasi 12 imetalekezwa kituo cha pilisi cha wilya ya Kahama.

Imeelezwa kuwa, wezi wa bastola hiyo walivunja kioo cha gari la mfanyabiashara, Renatus Lucas (44) mkazi wa mtaa wa Mbulu, mjini na kuiba bastola pamoja na fedha taslimu laki sita za kitanzania.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema tukio hilo lilitokea saa nne usiku wakati mfanyabiashara huyo alipukuwa ameegesha gari lake nje ya hoteli na kuenda kula chakula.

Amesema baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa mfanyabiashara huyo mara moja walianza kuendesha msako mkali na kufanikiwa kukuta silaha hiyo imetelekezwa na wezi eneo la polisi,

Kamanda Magiligimba amesema polisi wanamhoji Lucas kwa tuhuma ya uzembe wa kushindwa kutekeleza wajibu wa kulinda silaha yake na kusababisha kuibiwa.

DC Mjema afunguka wagonjwa wa Corona kutoroka Amana
Serikali yatangaza kibano mitandao ya kijamii, vyombo vya habari vinavyovunja sheria