Kaimu Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA Kanda ya Kati, Christian Mbwasi, amewaomba Wazee wa Kimila na Machifu nchini, kwa nafasi zao kupinga matumizi ya dawa za kulevya, ili kuiokoa jamii.

Kamishna Christian ametoa ombi hilo wakati akizungumza na Viongozi hao kutoka kanda ya Kati Dodoma na kanda ya Pwani kwa Mkoa wa Morogoro na Zanzibar, aliposhiriki kwenye sherehe za kimila zilizofanyika viwanja vya machifu eneo la bwibwi – Njedengwa Dodoma.

Amesema, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, inaamini kupitia sauti za wazee wa kimila, kwa umoja wao wataweza kuiokoa jamii kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya huku akiwataka kuukumbusha umma juu ya athari za kujihusisha na matumizi au kilimo cha bangi na mirungi, hali inayohatarisha ustawi wa Taifa.

“Nyinyi ni viongozi wa jamii, tunaamini kwa kupitia sauti zenu ujumbe wetu utafika kwa haraka kuhusiana na kuitaka jamii kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya hivyo tunao wajibu wa kuhakikisha kwa pamoja tunaiondoa hali hiyo,” alisema Kamishna Christian.

Uhusiano wa Misri, Zanzibar ni mzuri - Balozi Mbarouk
Danny Drinkwater atundika daluga