Bao la mshambuliaji Jermain Defoe liliifanya klabu ya Bournemouth kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brighton and Hove Albion ukiwa ni ushidi wa kwanza kwa klabu hiyo msimu huu.

Katika mchezo huo uliopigwa jana katika uwanja wa Vitality, Brighton walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Solly March katika dakika ya 55 kabla ya Andrew Surman kuisawazishia Bournemouth bao hilo dakika ya 67.

Mshambuliaji Jermain Defoe aliyesajiliwa msimu huu kutoka Sunderland alipachika bao dakika ya 73 na kuifanya Bournemouth kupata ushindi wa kwanza baada ya kufungwa katika michezo yote minne ya awali waliocheza kwenye ligi kuu msimu huu.

Hata hivyo pamoja na ushindi huo Bournemouth bado inabaki katika nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na pointi 3 tu huku Crystal Palace wakiburuza mkia nafasi ya 20 wakiwa wamecheza michezo minne na kufungwa michezo hiyo yote.

Defoe ameifungia Bournemouth bao la kwanza tangu mwaka 2001 (siku 5977zilizopita) alipofungia timu hiyo ikicheza dhidi ya klabu ya Reading.

 

 

 

 

 

 

Video: Balaa laanza kibano makinikia, Maombezi ya Tundu Lissu ngoma nzito
Dunia kushuhudia pambano la mwaka la masumbwi leo, Canelo Vs Triple G