Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani na kusema ameifungua Tanzania katika uhusiano wa kimataifa, Demokrasia na ukuaji wa Uchumi kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sheikh Alhad Mussa Salumu amesema kwa sasa wanasiasa wote wana furaha baada ya uwepo wa maridhiano na wameondoa uoga uliokuwepo wa kufanya siasa zao katika maeneo mbalimbali ya nchi.
“sote tumeshuhudia Rais amefungua eneo la siasa na kuifanya Demokrasia kwamba sasa imekuwa pana huu ni ukomavu wa kisiasa, hata alipoudhuria mkutano wa Bawacha alipangua hoja baada ya hoja ya Mbowe na kuwasisitiza kila mmoja kushiriki kuijenga nchi,” amesema Sheikh Alhad.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Mchungaji Geogre Fupe amesema wa Rais Samia Suluhu Hassan umegusa nyanja zote za msingi kwa Taifa ikiwemo uwepo wa demokrasia imara, maendeleo ya ukuaji wa uchumi pamoja na uhusiano wa kimataifa.