Serikali ya Tanzania imesikitishwa na uamuzi wa nchi ya Dernmark kufunga shughuli za ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ameelezea masikitiko ya Serikali kufuatia hatua hiyo ya Denmark ikizingatiwa jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya 6 ya kufufua na kuimarisha diplomasia, uhusiano na nchi rafiki
Kwa upande wake Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Flemming Moller Mortensen, amesema haikua rahisi kufikia uamuzi huo ila kutokana na vipaumbele vya Denmark kama ilivyoanishwa kwenye mkakati wake mpya wa “The word We share” ni kuwa karibu zaidi na nchi zenye machafuko na migogoro hususani katika ukanda wa Sahel, Pembe ya Afrika na Nchi jirani za kanda hizo ambazo zina matatizo ya kisiasa.