Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’, amemjibu Haji Manara kwa kueleza uhalisia wa tajiri huyo.

Crescentius Magori, Mshauri wa Mohamed Dewji ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, amesema kinachoendelea kwa mtu mmoja kuzungukaa na kuzungumza upuuzi, hakitaiyumbisha klabu yao.

Magori amesema: “Kuna watu wanazunguuka kwenye Media na kusema Mohamed Dewji ni tajiri wa mitandaoni, eti kisa matajiri wengine hawaonekani mitandaoni, “
“Napenda kuwajibu kwamba hiyo ndiyo life style ya MO na mimi kama mshauri wake namshauri asibadilishe Style ya maisha yake kwa kuishi wanavyotaka watu wengine.”

“Tunajua yote yanaendelea huko ni kutaka kumdhoofisha Mohamed Dewji ‘Mo’ ili waidhoofishe Simba SC. Yaani ni propaganda za kizamani.”

“Niwahakikishie wamegonga mwamba Mohamed anasema hatotetereka wala hatoyumbishwa na maneno ya mtu yeyote, yeye anaijenga Simba SC ifike ambako inastahili pia amehaidi ni lazima Simba SC ya msimu ujao ipige hatua zaidi ya msimu uliopita. Na kuhusu Makombe tutachukua na Tutachukua tena.”

Magori ambaye alikua sehemu ya viingozi waliokuwa kambini nchini Morocco, kwa sasa yupo safarini kurejea jijini Dar es salaam.

Vituo maalum vya kuchoma chanjo ya Corona vyafunguliwa uwanja wa mkapa, uhuru
Denmark kufunga ubalozi wake Tanzania