Nikiangalia kiuhalisia Yanga haikwepeki kwenye kipindi chochote cha michezo katika vyombo vya habari. Hapa ninamaanisha kuwa katika vipindi hamsini vya michezo kwa siku, asilimia mia moja ni lazima waiongelee Yanga SC ama kwa mazuri au kutafuta mabaya ya Yanga.

Wanayanga hapa tunapaswa kuwa Proactive na hiki kitu mara nyingi huwa tunakikosa (Kuna sababu nyingi hapa). Yanga ina taarifa nzuri nyingi sana lakini zinazovuma ni mbaya, kwanini? Walaji wa taarifa za Yanga SC ni wengi, je taarifa tunazowapa zinajitosheleza?

Strategies gani za makusudi tunazo katika kuzuia taarifa mbaya za kila siku kwa Klabu yetu?! Klabu inaendeshwa na walaji wa taarifa mbaya au Club inawaendesha walaji kwa taarifa nzuri watakazo?  Yanga SC tumekuwa tukirudishwa nyuma sana na uvumi, taarifa mbaya na ugomvi ambao siku ya mwisho inaleta migogoro na kutuzuia focusing katika Mambo ya msingi kwa klabu yetu.

Ni muhimu klabu iwe na Idara ya kusimamia haya mambo, yaani ukiwa na taarifa mbaya za Klabu ya Upande wa pili huwezi kupata media zitakazokubali kurusha “Ujinga” wako, regardless ni ukweli au uongo. Kwanini Yanga SC taarifa zake ukitaka kuongea utatembezwa vituo mbalimbali vya media kuongea?! Tena utapata mpaka nauli kutoka “kusikojulikana”.

Wakati tunajiandaa kuelekea kwenye mchakato wa mabadiliko ya kiuendeshaji wa Klabu yetu ambao ni stage muhimu sana kwa kipindi cha miaka 85 ya Uhai wa Klabu yetu lazima tujiandae vizuri na kujilinda, hicho kitakuwa kipindi kigumu mno maana siyo wote watakaopenda tuvuke salama, lazima tuwe na mipango ya Kisasa na “kihuni” katika kuyalinda mabadiliko hayo ama sivyo tutatetereka sana!

Nilazima tujiandae nje na ndani, Yanga kila mtu anajua, sasa ni lazima tuwe hatua mbili mbele katika kusimamia mabadiliko ya Klabu.

Huu ni mtazamo ambao pia unapaswa kupelekwa katika idara ya Habari ya Klabu kwa mipango zaidi.

Jambo la kuonekana Makamu Mwenyekiti wetu amekosea halikupaswa kuzungumziwa vibaya nje bali tulipaswa kuonyana ndani badala ya sisi kuwa wakwaza kulitilia CHUMVU NA SUKARI… tunajikaanga kwa Mafuta yetu wenyewe kama SAMAKI.

Alichokifanya Makamu wetu Mwakalebela na namna tunayoitumia kumshambulia INA MADHARA ZAIDI KWA KLABU YA YANGA KULIKO MAKAMU MWENYEWE.

Ombi langu kwa Waandishi na wachambuzi wenye vinasaba vya KWELI na Yanga ni Angalieni ni maeneo gani mnaweza kuipigania Klabu yenu kwa uwezo na nguvu zenu zote. Wenzetu wamekuwa wakikosea sana na hata kutukana kwa matusi mitandaoni lakini walikaa kimya kabisa na mambo yakapita bali sisi ndio tunashinda nayo na kuamka nayo kwa kushindana kuandika.

Je kwa kufanya hivi tunajenga nini kwa Timu yetu kuelekea kwenye Mabadiliko ya Kimfumo?

Hapa  nimetoa mawazo yangu ambayo nadhani kwa pamoja tunaweza kusimama vizuri!

Deo Mutta

Mwanachama Wa Yanga

Kenya: Asiyevaa barakoa kwenda jela miezi 6
Lusajo asitisha mpango wa mkataba mpya Namungo FC