Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania SAPC Fortunatus Muslim ametangaza kumfungia leseni kwa miezi sita, dereva Said Abbas baada ya kusababisha ajali mlima Kitonga.
Amesema uamuzi wa adhabu hiyo umefikiwa baada ya Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kufanya uchunguzi na kubaini chanzo cha ajali hiyo ambayo iliua watu 10.
Takribani siku nne zilizopita, basi la PRESDAR lilipata ajali kwa kuacha njia na kupinduka katika mlima Kitonga wilayani Kilolo mkoani Iringa ambapo dereva wa gari hilo alipona.
Akizungumza katika eneo la tukio, Muslim amesema Jeshi hilo limefuatilia kwa karibu tukio hilo kwa maana ya kufanya uchunguzi na kubaini chanzo cha ajali hiyo ni uzembe ambao ungeweza kuzuilika endapo taratibu za tahadhari zingechukuliwa mapema na dereva.