Ikiwa ni siku chaghe tangu zitolewe taarifa za utoroshwaji madini kilo 6.93 Oktoba 26, 2023, Madini mengine yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 961 Milioni yakiwa na uzito wa Kilogramu 6.93 yamekamatwa Wilayani Chunya Mbeya, yakitoroshwa kwenda kuuzwa nje.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, katika machimbo ya dhahabu Wilayani Chunya amewataka Wafanyabiara wa madini, kutojihusisha na njama za utoroshaji madini.

Amesema, Wizara ya Madini ina mikakati mbalimbali ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapatia mitambo ya uchorongaji , kuwajengea mazingira wezeshi ya kupata mikopo yenye riba nafuu na kufanya utafiti wa kina, ili kufanya uchimbaji bila kubahatisha.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mayeka Mayeka amesema mazingira ya uchimbaji madini Wilayani Chunya yanaendelea kuimarishwa ingawa zipo changamoto za utoroshaji madini na wizi wa Carbon katika mialo ya uchenjuaji madini.

Awali, akitoa taarifa kuhusu Sekta ya Madini Wilayani Chunya Afisa Madini Mkazi, Sabahi Nyansiri amesema mpaka sasa vituo vidogo 24 vya ununuzi wa dhahabu vimefunguliwa, ili kusogeza huduma ya ununuzi na uuzaji kwa wachimbaji wadogo wasio na uwezo wa kufika katika soko kuu.

Kairuki ataka ubunifu wa kazi TAWIRI
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 29, 2023