Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina, Angel di Maria amewasili mjini Doha, nchini Qatar kwa lengo la kukamilisha uhamisho wake kutoka Man Utd, kuelekea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa,  Paris Saint-Germain.

Mshambuliaji huyo anatarajiwa kukamilisha mpango wa kuhamia PSG hii leo na tayari kiasi cha paund milioni 44.4 kinatajwa kama ada yake ya uhamisho kutoka Old Trafford mjini Manchester nchini Uingereza.

Jana jioni mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, aliweka picha katika akaunti zake za mitandao ya kijamii, akionyesha namna alivyowasili na kupokelewa na wenyeji wake huko mjini Doha, ambapo ndipo nyumbani kwa mmiliki wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi.

Di Maria, aliwasili mjini Doha akitokea moja kwa moja nchini kwao Argentina akipitia mjini Sao Paulo nchini Brazil kutokana na safari ya ndege aliyokua amepanda.

Hii leo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake katika kituo cha Aspire centre na itakapothibitika amekidhi vigezo vinavyotakiwa na PSG atasaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.

Diego Costa Kuwakosa Swansea City
Dk. Slaa Asema Anatishiwa Maisha, ‘Mapenzi Ya Mungu Yatimie’