Msanii wa muziki nchini, Diamond Platinumz anategemea kutoa msaada mkubwa kwa familia 500 ambazo ameahidi kuzilipia kodi ya nyumba kwa miezi mitatu kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 ambao umeathiri uchumi wa watu wengi.
Ameongezea kuwa siku ya Jumatatu atangaza utaratibu atakaotumia kugawa msaada huo kwa familia hizo 500 huku akienda na kauli mbiu isemayo ”Tatizo lako ni tatizo langu, pamoja tunaweza kupambana dhidi ya Corona, Hili pa litapita”.
Amesema hayo kwenye ukurasa wake Intagram wenye zaidi ya wafuasi milioni 9, Diamond ameandika.
”Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu, ijapokuwa na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho nitoe kusaidia kulipia kodi za nyumba kwa miezi mitatu kwa familia 500 walau kusaidia katika kipindi hiki kigumu cha kupamba na virusi vya corona” ameandika Diamond.
Aidha huu umekuwa utaratibu wa watu wengi maarufu duniani kusaidia jamii hasa katika kipindi ambacho nchi zao zinakabiliwa na majanga ambayo yameleta athari kubwa.
Tukio kama hilo limetokea nchini Marekani ambapo mmiliki wa nyumba aliyefahimka kwa jina la Mario Selerno aliamua kuwasamehe kodi wapangaji wake zaidi ya 200 akishirikiana nao katika harakati za kupambana na janga hili la corona lilioikumba dunia na kusababisha maafa makubwa ya kiuchumi.