Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (Nacopha), limetoa vifaa vyenye thamani ya Tsh. milioni 26 kwa mkoa wa Tabora kwaajili ya watu wanaoishi na virusi hivyo ili wajikinge na maambukizi ya virusi vya Corona.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa jana na mtendaji mkuu wa Nacopha, Deogratis Rutatwa kwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Manri kwaniaba ya halmashauri zote za mkoa huo.

Msaada huo wameshirikiana na shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID), chini ya kauli mbiu ‘Hebu tuyajenge tufikie 95-95-95’ na kuunga mkono jitihada za srikali za kudhibiti maambukizi ya corona kwa watu wanaoishi na VVU.

Rutatwa amesema wametoa vifaa hivyo kwaajili ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ili waweze kujikinga wasipate maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (covid -19).

Mikoa mingine ambayo imefikishiwa vifaa hivyo ni Kigoma, Shinyanga, Geita, Kagera, Mwanza na Mara.

Diamond ajitosa kulipia kodi familia 500
Ni Kweli Kim Jong-un amefariki dunia? Trump haamini, ‘Marekani’ waanza sherehe mapema!?