Diamond Platinumz amezungumzia mpango wa kufanya filamu za Kiswahili maarufu kama ‘Bongo Movies’.

Msanii huyo mwenye umaarufu mkubwa barani Afrika amesema kuwa soko la filamu Tanzania bado halimshawishi msanii kama yeye kujiingiza katika tasnia hiyo.

“Nipo kimaslahi zaidi, mimi nafanya muziki kutafuta pesa, uigizaji hapa Bongo bado haujafikia hatua inayoridhisha kumwezesha msanii kama mimi kujihusisha nayo,” Diamond aliliambia gazeti la Mwananchi.

Hata hivyo, alikiri kuwa anatambua uwezo wake katika sanaa ya maigizo na kwamba endapo soko la filamu litaanza kulipa kwa kiwango kinachoshawishi ataweza kuingia.

“Ni kazi ngumu lakini masilahi madogo. Sio kama sipendi au siwezi kuigiza, lakini nitaweza kufanya hilo wakati filamu zikilipa, huko pia nitaingia.”

Diamond Bongo Movies

Diamond amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na muigizaji wa Bongo Movies, Wema Sepetu pamoja na Jokate Mwegelo hivyo anaweza kuwa anafahamu kwa undani baadhi ya mambo yaliyoko kwenye tasnia hiyo mbali na kipato.

 

Zitto Kabwe Ampa Rais Magufuli Ushauri Mgumu
Kofia Ya 'M4C' Yatajwa Kama Kigezo Cha Kumvua Ubunge Peter Msigwa