Baada ya kufanikiwa kuvunja Rekodi yake mwenyewe, Mlinda Lango chaguo la kwanza la Young Africans Djigui Diarra amesema anafurahi kuendelea kuimarika huku akitaja siri, ni kuzoea ligi na ubora wa safu yake ya ulinzi.

Mlinda Lango huyo kutoka nchini Mali amefikisha clean sheet ya 16 akizidi moja tu ya msimu uliopita ambao alimaliza na 15.

Diarra zikiwa zimebaki mechi tatu kwa kila timu ili kukamilisha msimu tayari ametangazwa kipa bora wa msimu kutoka na na kuwa na clean sheet 16 hadi sasa ambazo haziwezi kufikiwa na kipa yeyote.

Diarra amesema “Nafikiri pia nimeshazoea ligi ya Tanzania msimu wangu wa kwanza kucheza nilifanya vizuri na naendelea kufanya hivyo, sio rahisi ni juhudi binafsi na kusaidiwa na ukuta imara unaojengwa na timu yetu”

“Kilicho fanyika msimu huu kufikisha clean sheet 16 nikiwa na mechi tatu mkononi natamani pia msimu ujao niendelee kupanda juu ya hapo na sio kuteremka kwani kuwa bora langoni kunaniongezea sifa zaidi kwenye ligi ya Tanzania.” amesema

Diarra alitumia nafasi hiyo kulishukuru benchi la ufundi la timu hiyo kuweza kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza na kuahidi kuendelea kuwa imara zaidi ili kujitengenezea rekodi yake mwenyewe kwenye ligi ya Tanzania.

Akizungumzia mechi ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani African dhidi ya Marumo Gallants mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumatano (Mei 10), Diarra amesema ni mchezo muhimu kwao ambao utaendelea kuwajengea heshima wamejiandaa kuhakikisha wanavuka hatua inayofuata.

“Sio mchezo rahisi tunatambua umuhimu wake, benchi la ufundi pia linatambua nini kinatakiwa kufanyika hivyo tutaingia kwa kumheshimu mpinzani wetu na kutumia vyema uwanja wetu wa nyumbani kupata matokeo mazuri,” amesema Diarra

Hizi hapa sababu za Mandonga kupelekwa Dodoma
Fadhili Majiha kumsindikiza Mfaume Mfaume