Zogo la malumbano kati ya wakala wa kiungo kutoka nchini Ivory Coast Yaya Toure na meneja wa Man City Pep Guardiola, huenda linaibuka kwa mara ya pili, kufuatia mgongano wa kauli zilizotolewa na wawili hao.

Dimitry Seluk wakala wa Toure, ameandika katika ukurasa wa akaunti yake ya twitter akieleza utayari wa mchezaji wake kucheza katika kikosi cha kwanza kwa kigezo cha kuwa umbo zuri, tofauti na inavyodhaniwa, kufuatia kauli iliyowahi kutolewa na Guardiola mbele ya waandishi wa habari kwa kusema kiungo huyo anajua sababu za kutopangwa katika michezo waliyocheza tangu msimu huu wa 2017/18 ulipoanza mwezi uliopita.

Inadhaniwa huenda Toure kawa na umbile kubwa (Kibonge) kwa sasa, hali ambayo inamfanya Guardiola kushindwa kumtumia katika kikosi chake, kutokana na utetezi uliotolewa na wakala Seluk.

Ujumbe wa Seluk katika tweeter umesomeka: “Yaya ana umbo zuri. Atathibitisha hilo. Yupo tayari kucheza. Ni maamuzi ya Guardiola kumtumia.

Msimu uliopita Seluk alitibuana na Guaradiola kwa sababu za mchezaji wake kushindwa kutumika kikamilifu kwenye kikosi cha kwanza, hali  ambayo ilimfanya meneja huyo wa zamani wa FC Barcelona kutangaza hadharani kuombwa radhi na Yaya Toure, jambo ambalo lilifanyika miezi kadhaa baadae.

Pasipoti za kielektroniki kuzinduliwa rasmi
Video: Man City, Real Madrid zang'ara, Liverpool yabanwa