Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania hii leo Desemba 9, 2023 yameambatana na Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ametumia mkutano huu kuulezea umma umuhimu wa dira ya maendeleo ya Taifa.

Katika hotuba yake, Rais Samia amesema, ‘’Dira ya maendeleo ni andiko maalum linaloainisha mipango iliyowekwa, mikakati itakayotekelezwa na raslimali zitakazotumika katika kipindi kitakachowekwa ili kufikia malengo yanayokusudiwa ya maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.”

Amesema, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2020-2025 ilijengwa kwa nguzo kuu nne ambazo ni kuboresha hali za maisha za Watanzania, kuwepo kwa mazingira ya utulivu,amani na umoja, kujenga utawala bora na utawala wa kisheria na kujenga uchumi imara unaoweza kuhimili ushindani kutoka mataifa mengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Taifa kwasasa linajitosheleza kwenye chakula kwa asilimia 124 na lengo likiwa ni kufikia asilimia 140 ifikapo mwaka 2025. Matarajio ya Dira itakayoandikwa ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha chakula kwa ajili ya bara la Afrika na kwingineko duniani,” alisisitiza Rais Samia.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini, Vyama vya Siasa na Wananchi.

Mbio za Mtumbwi zahitimisha sherehe za Uhuru Kagera
Uhuru wa Tanganyika: Kilimanjaro hawakujua maana