Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere huenda akaondoka kaskazini mwa jijini London na kutimkia nchini Uturuki kujiunga na Trabzonspor kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, anapewa nafasi hiyo, kutokana na mambo kumuendea kombo katika kikosi cha Aresene Wenger, kufuatia kukosa fursa ya kucheza tangu msimu huu ulipoanza.
Dirisha la usajili nchini Uturuki bado lipo wazi, na Trabzonspor wana matumaini ya kumpata Wilshere kwa kuwasilisha ofa ambayo huenda ikampendesha Arsene Wenger.
Hata hivyo Wilshere, tayari ameshasajiliwa kwenye shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kwa ajili ya michuano ya Europa League, lakini hatua hiyo haitomzuia kuondoka.
Msimu uliopita Wilshere alipelekwa kwa mkopo AFC Bournemouth, kufuatia changamoto za kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal.