Mkuu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania Dk. Fredrick Shoo amewataka wananchi kuchua tahadhari zote na maelekezo yanayotolewa na serikali juu ya kujilinda na maambikizi ya virusi Corona na kutambua wajibu wa kujilinda na kuwalinda wengine.
Shoo ameyasema hayo leo April12, 2020 Katika ibada ya Pasaka usharika wa Moshi mjini Dayosisi ya kaskazini ya kanisa hilo ambapo ansema ni wakati wa Kila mmoja wa kumita na kumomba Mungu ili aweze kuliondoa taifa Katika janga la Corona ambalo Kumekuwa tishio duniani kite.
“Tuchukue tahadhari zote na kufuata maelekezo Lakini tusiache kumtazama huyu yesu aliye na nguvu na tumaini letu lililo kuu kuliko yote tumuombe sasa huyu Yesu mfufuka aturejeshee tena amani tumaini atupe uhai na kutukinga hatari zote, hata janga hili la Corona ambalo limeachilia hofu na huzuni duniani” amesema Shoo.
Aidha amesema tutoke hapa tukiwaambia watu corona ipo tujihadhari lakini Yesu kristo yupo ambae ni mshindi wa Kifo na mauti tuendelee kumuomba na kumuita Mungu maana yeye mwenyewe aliahidi tukimuita atatuitikia na kutuonyesha mambo makubwa na magumu tusiyoyajua.
Hata hivyo Dkt.Shoo amesema kuwa wananchi wote wakiungana kwa pamoja kuchukua tahadhari na kuzingatia maagizo yanayotolewa Katika kuzuia virusi vya Corona kuenea na kumomba kwa pamoja Mungu atasikia na kuiponya nchi.