Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa wakati, Edward Lowassa alipotaka kurudi ndani ya chama hicho, walimtaka kiongozi huyo kwenda kuomba ridhaa kwenye ngazi ya tawi, na wakimridhia ndipo aweze kurejea.
Dkt. Bashiru Ally ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo suala la miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema kuwa kuhusu wanasiasa waliorudi CCM sharti la kwanza lilikuwa wakubaliwe uanachama kwenye tawi suala ambalo ni sifa mojawapo ya kuweza kukubalika katika chama.
“Lowassa kurudi Chama Cha Mapimduzi (CCM) kulikuwa na mazungumzo ndani ya chama baada ya kupokea maombi yake na wala hakuwa yeye peke yake,”amesema Dkt. Bashiru.
Aidha, Machi 1, 2019 katika Makao Makuu madogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam, Edward Lowassa alitangaza uamuzi wa kurejea CCM baada ya kuondoka wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015.