Wanaoomba vibali wanaoomba vibali vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati majengo na badala yake wanafanya ujenzi bila kuzingatia mipango kabambe ya uendelezaji miji katika maeneo husika waonywa.
Onyo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ameonya wanaoomba vibali vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati majengo na badala yake wanafanya ujenzi bila kuzingatia mipango kabambe ya uendelezaji miji katika maeneo husika.
“Tunahitaji kutengeneza miji yetu hatuhitaji kurudi nyuma, gharama iliyotumika kwenye uandaaji master plan ni kubwa sana, sasa haiwezekani kujengwa nyumba mpya katika eneo lenye mastaer plan” amesema Dk Mabula.
Ameagiza wakurugenzi na makamishna wa ardhi wasaidizi wa mikoa kuhakikisha wanapita na kukagua kama kuna vibali vipya vilivyotolewa na ujenzi kufanyika kinyume na mipango kabambe ya uendelezaji miji kusitishwa mara moja.