Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema wapo baadhi ya viongozi ambao kwa maslahi yao binafsi wanachangia uharibifu wa mazingira na kwamba haamini wale wanaowachunga ng’ombe ndiyo wamiliki halali wenye kuviharibu na vyanzo vya maji.

Dkt. Mpango, ameyasema hayo hii leo Desembalse 19, 2022 katika Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na Utunzaji wa vyanzo vya maji, na kusema viongozi wa namna hiyo hawafai kwa kuwa wanaweka rehani maisha ya watanzania na kwamba Serikali haiwezekani kuacha tabia hiyo iendelee kwakuwa ina madhara kwa jamii.

Amesema, “Ni lazima kuwa na juhudi katika kushirikiana na wadau, Serikali selta binafsi na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mazingira yanalindwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya maisha ya watanzania na viongozi embat wao wanashiriki kufanya uharibifu niwaambie hawatufai.”

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa, kama ilivyokuwa katika vita ya wazee wetu hapo zamani ambapo waliungana kuupinga ukoloni, ndivyo kwasasa inahitajika jamii iungane kupinga uharibifu wa mazingira na kutaka kila mkoa kuwa na jitihada za kupanda miti rafiki wa mazingira kama moja ya mikakati yente muleta tija.

Aidha, amesema kongamano hilo limekuja wakati muafaka na limekuwa ni muhimu kwani linajadili, kupanga na kuweka mkakati wa uhifadhi mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa ajili ya matumizi ya jamii na kiuchumi na kwamba bonde la mto Ruaha linatakiwa kulindwa kwa nguvu zote.

Hata hivyo, amewakumbsha viongozi wa Mikoa kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya Serikali na kusimamia maslahi ya nchi kiujumla na kuwapongeza Waandishi wa Habari kuendelea kuihamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 20, 2022
Wananchi watakiwa kutunza mazingira