Wakulima na wafugaji kutunza mazingira ili kuendelea kupata mvua za kutosha, kwani wamekuwa wakiharibu mazingira na vyanzo vya maji kwa kilimo na ufugaji ambao hauna tija kwa wananchi wengi kwa kuwa wamekuwa wakiharibu mazingira bila sababu ya msingi.

Hayo yamesemwa na Kamishina wa uhifadhi wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. DoS Santos Silayo.

Prof Silayo amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuendelea kuvitunza vyanzo vya maji na mazingira kwa faida ya Taifa na dunia kwa ujumla.

Kamishna wa uhifadhi wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof DoS Santos silayo

Aidha amewataka wananchi kuwapinga vikali wananchi wengine ambao wamekuwa wakiharibu mazingira kwa makusudi na kusababisha majanga kwa binadamu na wanyama.

Prof Silayo amesema kuwa mazingira yakitunzwa vizuri yanakuwa na faida kubwa katika maisha ya binadamu na viumbe vingine ambavyo kwa kiasi kikubwa wanategemea mazingira mazuri na bora.

Viongozi wenye maslahi binafsi hawatufai: Dkt. Mpango
Siku ya 130 Ruaha Mkuu hautiririshi maji