Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Malengo ya Maendeleo Endelevu unaofanyika jijini New York nchini Marekani, akiambatana na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Matifa, Balozi Hussein Katanga na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk.

Dkt. Philip Mpango aliwasili Jijini New York kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa – UNGA78.

Aidha, Makamu huyo wa Rais ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano mbalimbali inayohusu Mazingira, Uchumi, Afya, Maji, Demokrasia na Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambapo Tanzania imealikwa na Nchi washirika, Taasisi za kimataifa na Asasi binafsi.

Dkt. Mpango pia anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani Septemba 21, 2023 na tayari ameanza kushiriki Mikutano mbalimbali ikiwemo ule wa jana (Septemba, 18, 2023), wa ufunguzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa.

Uchumi: Serikali kujenga Kiwanda cha kubangua Korosho
Serikali yaagiza watumishi sita wachukuliwe hatua