Ikiwa leo ni siku ya pili ya mkutano wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum), nchini Ufaransa Makamu wa Rais ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Julai 1, anatarajiwa kutoa ahadi za Tanzania katika Jukwaa hilo.

Aidha Dkt. Mpango anatoa ahadi hizo katika kipindi ambacho Tanzania inaonekana kama kinara wa uwezeshaji Wanawake kiuchumi kama ilivyoridhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Jukwaa hilo lenye madhumuni ya kuchagiza usawa wa kijinsia, linajadili umuhimu wa uwezeshaji Wanawake kiuchumi kama nyenzo ya kumnyanyua Mwanamke kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Pia Mwanamke kupata Teknolojia rahisi na sahihi katika kufanya shughuli za kiuchumi, kutolewa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na utoaji wa mitaji kwa Wanawake pamoja uwepo wa mifumo sahihi ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Wanawake.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo.

Nugaz: Young Africans hatudhulumu
Pigo benchi la ufundi Simba SC