Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amefanya ukaguzi wa masoko Wilaya ya Temeke Leo Juni 28, 2021 ili kuona changamoto zinazoikabili masoko hayo

Akiwa katika ziara hiyo, RC Makalla ameainisha moja ya changamoto kubwa kuwa ni daladala kutokufika katika maeneo ya masoko ikiwemo soko la kijichi na kuagiza zitatuliwe haraka.

Katika kutoa maagizo hayo, RC Makalla amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo kuwaelekeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha ndani ya wiki moja daladala zinafika kwenye soko la Kijichi ili kuchagiza biashara sokoni hapo.

“Nimekuja na Mkuu wa Wilaya yeye ndio Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama, LATRA wapo tunataka mabasi yaje hapa DC Simamia, LATRA waite na mimi naagiza ndani ya wiki moja nitakuja nataka kukuta daladala hapa, tusibembelezane dalala zije hapa shida nini watu wakishuka hapa watanunua kitu cha kwanza, watatamani na kitu kingine,” amesema RC Makalla.

Sambamba na hayo, RC Makalla amesema baadhi ya watendaji ndio wanakwamisha masoko kutokana na kutokuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo katika masoko, huku akisema kuwa baadhi ya ubunifu kwenye masoko hauzingatii utamaduni wa kitanzania.

TBS yasisitiza matumizi huduma zenye ithibati
Vyombo vya Habari kulipiwa Bilioni 6