Serikali kuvilipia vyombo vya habari deni la zaidi ya bilioni 6 baada ya kufanya uhakiki wa deni hilo ambalo ni moja ya sababu vyombo vya habari vingi kufa.

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati akijibu swali la Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Deodatus Balile.

Balile alimuomba Rais Samia kutamiza ahadi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kulipa deni kabla ya Juni 30, 2021.

Rais Samia amesema kuwa Serikali itafanya uhakiki wa madeni hayo ya vyombo vya habari, kisha itaanza kulipa kidogokidogo mpaka deni hilo liishe.

“Nitafanya kazi na waziri mkuu katika kuhakikisha kwamba tunalipa madeni haya kidogokidogo lakini lazima tuyafanyie uhakiki kisha tuweze kulipa, hatutaweza kulipa kwa mkupuo,” amesema Rais Samia

“Wakati wangu huu sitakataza matangazo kwenye vyombo binafsi, kwa hiyo ni jukumu letu kutafuta matangazo hayo,” amesema Rais Samia.

RC Makalla atoa wiki moja magari yafike soko la Kijichi
Sirro kuteta na Waziri Mkuu