Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwasababu deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.
Amesema kuwa katika tathmini iliyofanyika mwezi Novemba mwaka huu inaonyesha kuwa uwiano wa deni hilo na pato la Taifa ni asilimia 32.5 likilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.
“Katika kuangalia ukomo wa deni hili ambao uko chini, inaonyesha kuwa deni hili ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na muda mrefu”, amesema Dkt. Mpango
-
Familia ya Babu Seya yamsaka Magufuli
-
Wanaume wanunua machangudoa sasa kutiwa mbaroni
-
Majaliwa awaweka kitimoto viongozi Tanesco
Hata hivyo, Mpango ameongeza kuwa Serikali tangu ifanikiwe kuziba mianya ya rushwa na ufisadi imefanikiwa kukusanya trilioni 1.2 kila mwezi na amewapongeza walipakodi nchini na kuwataka Watanzania kujenga tabia ya kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.