Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni mambo muhimu kwa nchi zinazoendelea hasa katika masuala ya uchumi wa kijamii kwa vile nchi hizo zinaweza kubadili maisha ya watu wake kupitia sekta muhimu kama ya kilimo, nishati na elimu.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipohutubia katika Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Kundi la 77 pamoja na China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unaofanyika katika ukumbi wa mkutano, Havana Cuba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Amekumbusha namna nchi zinazoendelea zilivyoathirika vibaya na janga la maradhi ya UVIKO-19, kwa kupanda kwa bidhaa, mizozo ya kisiasa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi na kudai kuwa hizo ni baadhi ya changamoto zilizosababisha kupanda kwa gharama za maisha na kudhoofisha jitahada za kujikwamua kiuchumi kwa nchi zinazoendelea.

Aidha, Dkt. Mwinyi pia alikumbushia namna nchi zilizoendelea zilivyobaniwa teknolojia ya kutengeneza chanjo nchi za mataifa ya kusini na kuzinyima kabisa msaada wa kiteknolojia ili ziweze kutengeneza chanjo, hali hiyo iliyosababisha makampuni ya utengenezaji dawa ya mataifa tajiri kujipatia faida kubwa kwa kuziuzia nchi masikini chanjo ya UVIKO-19.

Gamondi afunguka DR Congo ilivyomsaidia
Simamieni sheria ukomo matumizi ya Kemikali - Mitawi