Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakuisudia kutimiza ahadi na malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025, ya kuzalisha fursa mbalimbali za ajira ikiwemo uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na kuandaa mazingira wezeshi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akifungua Tamasha la kwanza la Fahari ya Zanzibar na mwaka mmoja wa Taasisi ya Wakala wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, Serikali imeendelea na hatua za kuimarisha miundombinu ya mazingira ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali ikiwemo ujenzi wa masoko na vituo vya mabasi na kwamba uchumi wa Zanzibar una fursa nyingi za masoko kwa kuwepo kwa Hoteli nyingi za kitalii kwa mahitaji ya bidhaa mbalimbali.
Aisha, amewataka wadau wanaojihusisha na sekta ya utalii kuhakikisha wajasiriamali wazawa wananufaika na fursa hizo na kutoa wito kwa wajasiriamali hao kuzalisha bidhaa kwa viwango vinavyohitajika ili kupunguza uingizaji wa bidhaa za nje ili kuimarisha soko la ndani.