Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kislamu kutumia uwepo wa misikiti katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kijamii.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Oktoba 7, 2022 baada ya ufunguzi wa msikiti wa Mubarak uliopo Kiboje Mwembeshauri Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema, katika jamii kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo watoto yatima, walemavu na wajane hivyo makundi hayo yanahitaji kupatiwa misaada kupitia misikiti.
Awali, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi amewataka wakazi wa kijiji cha Kiboje kutumia vizuri msikiti huo katika kujenga umoja na upendo kati yao, na kufundishana mambo mema.