Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mara baada ya uchaguzi kumalizika, ni muhimu kwa Chama na Wanachama kujenga umoja, kwa kuondoa makundi yote na kushirikiana kwa pamoja.
Mwinyi ameyasema hayo katika mkutano wa viongozi wa CCM ngazi ya Shina , Majimbo , Wilaya na Mkoa katika ziara yake ya kukiimarisha chama na kutembelea miradi mbalimbali ukumbi wa Picadilly, Kombeni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, “Wale ambao wanaendelea kukiuka taratibu na kuchangia kuwepo kwa makundi wanapaswa kuitwa na kuchukuliwa hatua na kamati za maadili ili kuhakikisha nidhamu na mshikamano ndani ya chama.”