Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amevunja bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Meli na uwakala Zanzibar ikiwa ni siku moja baada ya kutengua uteuzi wa Katibu wa Rais, Suleiman Ahmed Saleh.
Taarifa ya utenguzi huo imetolewa leo Desemba 15, 2020 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi wa Zanzibar Dkt. Abdulhamid Mzee.
Hatua hiyo ya kuivunja Bodi hiyo imechukuliwa kutokana na serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kutoridhishwa na uendeshaji na utendaji wa shirika hilo.