Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo, Mei 2, 2020 amemteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, uteuzi huo wa Dkt. Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi unaanza leo.

Dkt. Nchemba anachukua nafasi ya Balozi, Dkt. Augustine Mahige ambaye alifariki dunia jana, Mei Mosi, 2020.

Mtoto auawa kwa kushambuliwa na fisi nyumbani
Makamu wa rais aongoza mazishi ya balozi Mahiga