Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua kampeni za Chama cha mapinduzi katika uchaguzi mdogo jimbo la Longido unaotarajiwa kufanyika January 13, 2018 na kusema kwamba wapinzani wameogopa kushiriki kwa sababu wataachwa mbali sana.
Ameyasema hayo wakati akizindua kampeni hizo, Dkt. Nchemba amewataka wananchi wa jimbo la Longido kumchagua mgombea wa CCM Dkt. Steven Kiruswa awe mbunge wao kutekeleza ilani ya chama mapinduzi kwa kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.
Dkt. Mwigulu amesema wapinzani wameogopa kuwa wataachwa mbali katika baada ya kupima uitikio wa wananchi ambao wanakubali kazi za Rais John Magufuli na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na wananchi wanaona.
Hata hivyo, Dkt. Nchemba amewahakikishia wananchi wajitokeze siku ya kupiga kura kwani usalama ni wa uhakika wakati wa kupiga kura.