Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba ametahadharisha umma dhidi ya kauli mbalimbali zisizothibitika kuhusu usalama wa raia na mali zao zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Ameyasema hayo mjini Dodoma katika Mahojiano maalum na Mwandishi wa TBC1 ambapo pamoja na mambo mengine ni madai ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa, ambapo amesisitiza raia kutoa taarifa kwa vyombo vya dola wanapo hofia usalama wao.
Amesema kuwa yapo matukio yanayofanyika kwa ajili ya kuchafua taswira ya nchi hivyo amewataka wananchi kuwa makini na taarifa hizo.
Aidha, Dkt. Nchema amesema kuwa inapotokea miili inaokotwa baharini, bahari ambayo inachangiwa na nchi nyingi ambayo upepo unaweza kusafirisha miili kutoka sehemu mbalimbali, baadhi ya watu hudai kuwa watu wanauawa hovyo.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kila tukio linapotokea serikali huwa inachukua hatua na maisha ya watu yanapopotea sio vyema kuhusisha siasa, maana maisha yana thamani kubwa.