Mahakama moja ya mjini Istanbul, Uturuki imewahukumu waandishi wa habari 25 vifungo vya hadi miaka saba na nusu jela kwa kuhusishwa na kundi linalolaumiwa na Uturuki kwa kufanya jaribio la mapinduzi lililoshindwa mnamo mwaka 2016.

Ambapo wanahabari 23 wanahukumiwa kwa kupatikana na hatia ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi lililokuwa linaongozwa na muhubiri Fethullah Gulen wakati wengine 2 walishitakiwa kwa makosa madogo.

Wanahabari hao waliofungwa jela walihusika kufanya kazi katika chombo cha habari ambacho kina mahusiano ya karibu na muhubiri anayeishi Marekani Fethullah Gulen, ambaye serikali ya Uturuki inasema alipanga jaribio hilo la mapinduzi,

Tukio hilo la mapinduzi lililofanyika mwezi Julai 2016 ambapo liligharimu maisha ya watu 250 na kusababisha maafisa kadhaa wa serikali kukamatwa ambapo Fethullah Gulen amekanusha kuhusika na tuhuma hizo.

Maafisa wa Uturuki wamewaficha wanahabari kadhaa kufuatia msako uliofanywa baada ya mapinduzi hayo kushindwa.

Sio wanahabari wote wanatuhumiwa kwa kuwa karibu na muhubiri Gulen. Wengine wanaonekana kuziunga mkono harakati za wakosoaji wa Rais Recep Tayyip Erdogan.

 

Dkt. Nchemba awatahadharisha wanaotoa kauli 'tata'
JPM: Ninajua ukweli ni mchungu lakini lazima niwaambie