Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda baada vita kali aliyoifanya dhidi ya Wakuu wa Idara za Ardhi na kuwasimamisha kazi kwa utendaji wao mbovu sasa amehamia kwa wanaume wanaowapa wanawake ujauzito na kuwatelekeza.

Kufuatia tabia hiyo iliyozuka kwa baadhi ya wanaume mjini kukwepa majukumu yao ya malezi, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ameamua kuandaa jopo la wanasheria watakaoanza kuwachukulia hatua stahiki za kisheria wanaume wenye tabia hiyo watakao kuja kuripotiwa katika ofisi yake kuanzia Aprili 9, 2018.

Makonda amesema kitendo cha wanaume kukwepa majukumu ya malezi na matunzo kwa mtoto imepelekea pia baadhi yao kutoa ujauzito, kutupa watoto na wengine kupeleka wajukuu kulelewa na wazee na kusababisha mizigo kwenye familia.

Pamoja na hayo Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam amesena kwamba  ameamua kutoa muda wa mwezi mmoja ili kama kuna baba kwenye huu Mkoa anajijua ametelekeza mtoto na hatoi fedha za matunzo akamtafute na kuanza kutoa matunzo kwakuwa itakapofika Aprili 09  atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Zoezi hilo litafanyika kwa kushirikiana na kina mama wote waliotelekezwa na wanaume zao.

JPM: Ninajua ukweli ni mchungu lakini lazima niwaambie
Video: Wasiwadanganye muandamane, maana hamtabaki salama- Kamanda Mambosasa