Naibu Waziri wizara mambo ya nchi na ushirikiano wa Afrika ,ashariki Mhe, Dkt Damas Ndumbaru amekutana na kufanya mazungumzo na maseneta sita kutoka Ufaransa walioko kwenye ziara nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofis ndogo ya wizara Jijini Dar es Salaam ambapo ujumbe wa maseneta wa maseneta hao unangozwa na Mhe Herve Maury mwenyekiti wao ambaye pia ni rais wa kamati ya bunge ya mipango miji na maendeleo endelevu pamoja na balozi wa ufaransa nchini Mhe Frederic Clavier.

Katika mazungumzo hayo ujumbe wa maseneta umeeleza kuridhishwa na jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi kupitia uwekezaji kwenye miundombinu na kutunza mazingira

Kwa upande wake Naibu Waziri Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuuleza ujumbe huo sekta ambazo Tanzania inaweza kushirikiana na Ufaransa ili kukuza zaidi ushirikiano baina ya nchi hizi mbili uliodumu kwa muda mrefu

Ametaja sekta hizo kuwa ni pamoja na sekta ya kilimo, mifugo, madini, utafiti katika vyo vikuu pamoja na utalii na utunzaji wa mazingira.

”Katika kipindi hiki serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imeweka kipumbele kuendeleza kuendeleza viwanda hususa viwanda vya kuongea thamani”amesema  Dkt Ndumbaro

Aidha ameongeza kuwa Tanzania inamazingira ya uwekezaji na niwasihi tuu mtufikishie taarifa hizi kwa wawekezaji wanaoweza kuja kuwekeza nchini katika viwanda vya dawa na vifaa tiba pamoja na kiwanda cha kuunganisha magari.

 

Live: Makamu wa rais akifungua mkutano wa mawaziri wa kazi na Ajira SADC
Vijana 7 wafanyabiashara wafariki dunia kwa ajali mbaya