Mtafiti wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Haji Semboja amewataka watanzania kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kurudisha uzalendo na kudhibiti mianya yote ya ufisadi.

Amesema kuwa huyu ndiye Rais ambaye anayetakiwa kuiongoza Tanzania kwani ilipokuwa imefikia ni pabaya kwani kila mtu alikuwa anajichotea mali za umma bila mpangilio wowote.

Aidha, Dkt. Semboja ameunga mkono hatua iliyochukuliwa na Rais Dkt. Magufuli ya kuzuia mchanga kusafirishwa nje ya nchi kwani Taifa limekuwa ikiibiwa madini yake kwa muda mrefu huku kisingizio kuwa unaosafirishwa ni mchanga.

“Mimi ni kati ya Watanzania waliofurahishwa na maamuzi ya Rais, nina furaha kubwa hasa ukizingatia niliwahi kushiriki katika uandaaji wa sera za madini na uwekezaji, na ni wazi kuwa tumekuwa tukiibiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta ya madini, malalamiko haya  ya wizi na utoroshaji wa madini yamekuwepo kwa muda mrefu, kitu ambacho tulikua tukizungumza sasa kimethibitishwa baada ya Rais Magufuli  kupokea ripoti hiyo ya mchanga,”amesema Dkt.Semboja.

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 27, 2017
Video: Mtoto asimulia jinsi alivyowaokoa wenzake 9 kuzama ziwa victoria