Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ameongoza kikao katika Mkutano wa 18 wa Maspika na Viongozi wa Bunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika – CSPOC,

Kikao hicho, kimefanyika hii leo Julai 19, 2023, katika Ukumbi wa Mikutano wa Yaounde Jijini Yaounde Nchini Cameroon, ukijadilia masuala mbalimnali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Mkutano huo, ulifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Cameroon, Dion Ngute kwa niaba ya Rais wa Nchi hiyo, Paul Biya jana Julai 18, 2023.

Aidha, Dkt. Tulia yupo nchini humo akiwa ameambatana na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu pamoja na Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi.

Kuwa mpinzani sio kosa la jinai - Tundu Lissu
Serikali yataka weledi utokomezaji kero za ardhi