Mwanamke mmoja amewafungulia mashtaka rapa Drake na Future kwa madai kuwa alibakwa nyuma ya jukwaa na mtu aliyekuwa miongoni mwa timu ya tamasha lao la ‘Summer Sixteen’ mwaka jana.

TMZ imeripoti kuwa mwanamke huyo anawataka wasanii hao kumlipa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 25 ($25 million) kutokana na kitendo cha ubakaji alichofanyiwa kwenye tamasha hilo.

Akisimulia tukio hilo, mwanamke huyo alieleza kuwa alikuwa akijaribu kukutana na Future na Drake nyuma ya jukwaa huko Nashville, lakini alikutana na mwanamme mmoja ambaye alimueleza kuwa angeweza kumsaidia kukamilisha nia yake. Alisema wakati akipita katika moja ya sehemu za nyuma ya jukwaa hilo, mwanaume huyo alimsukuma ghafla na kuanza kumbaka.

Polisi wamemtaja mtuhumiwa kwa jina la Leavy Johnson mwenye umri wa miaka 38 ambaye alikamatwa mwezi Aprili na alikuwa akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.

Mwanamke huyo amedai kuwa amewaweka Drake na Future kwenye kesi hiyo kwakuwa wasanii hao pamoja na waandaaji wa tamasha hilo walipaswa kufahamu kuwa Johnson angeweza kuwa hatari.

Hata hivyo, wasanii hao hawajazungumzia tuhuma.

LIVE IKULU: Rais Magufuli, Rais wa Misri wakihutubia wananchi Ikulu Dar es salaam
Joselu Akaribia Kutua St James' Park