Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ anayecheza uzito wa Super Middle, amesema kuwa maandalizi ya pambano lake dhidi ya Erick Tshimanga Katompa wa DR Congo yamekamilika, hivyo mashabiki wake wasubiri burudani ya ngumi.

Pambano hilo lisilokuwa la ubingwa la raundi 10 linatarajiwa kupigwa Julai 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es salaam.

Mara ya mwisho mabondia hao kukutana ilikuwa Oktoba 9, 2021 pambano lililopigwa kwenye ukumbi wa PTA, Dar es Salaam na Dulla Mbabe kupoteza kwa pointi.

Majaji wote watatu walimpa ushindi Katompa, jaji Said Chaku alitoa 93-94 Theresia Kapinga 90-97 naye Pembe Ndava alitoa 93-94.

Dulla Mbabe, amesema anajua wapi alipoteleza hadi akapoteza pambano la kwanza ameyafanyia kazi mapungufu yake na anaamini kwa maandalizi aliyofanya anaamini anaenda kulipa kisasi chake.

“Najua mashabiki wangu wanatamani kuona nikienda kulipa kisasi na kufuta kile kilichotokea hapo awali nawaahidi kuwa pambano hili litakuwa la kutuma salamu kwa wengine wanaotamani kupanda ulingoni na Dulla,” amesema Dulla Mbabe.

Viongozi 10 waliozibeba nchi zao Afrika – Thomas Sankara
Richarlison afunguka sakata la Antonio Conte