Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, limefungua kesi ya kinidhamu dhidi ya klabu ya Dynamo Kiev kufuatia vurugu ziliziofanywa na mashabiki wa klabu hiyo, wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani humo dhidi ya Chelsea, uliochezwa usiku wa kuamkia juzi.

Katika taarifa yake UEFA imeeleza kuanza kusikiliza kesi hiyo utovu wa nidhamu itakapofika oktoba 27 mwaka huu.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa klabu ya Dynamo Kiev ya nchini Ukraine kuingia matatani, kwani waliwahi kufanya hivyo msimu uliopita na kusababishwa kutozwa faini pamoja na kuadhibiwa kucheza bila mashabiki.

Makossa yaliyopelekea adhabu hiyo kwa Dynamo Kiev, msimu uliopita yalikua ni vurugu pamoja na ubaguzi wa rangi.

Neymar Kuwakabili Argentina Pamoja Na Peru
Laana Ya Ufisadi Yaendelea Kuitafuna FIFA