Mshambuliaji wa klabu ya Man City, Edin Dzeko amewasili mjini Roma nchini Italia, tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya AS Roma mwishoni mwa juma hili.

Dzeko alipata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo inayotumia uwanja wa Olympico uliopo mjini Roma. Klabu hiyo inaamini ujio wa mshambuliaji huyo utakuwa chachu ya mafanikio wanayo yahitaji.

Uongozi wa klabu ya Man City tayari umekubaliana na As Roma ada ya usajili wa paund milioni 14, kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Bosnia na taratibu za malipo zitafanyika mara baada ya kukamilika kwa mipango ya vipimo vya afya.

Dzeko, ameelekea nchini Italia huku akiacha kumbukumbu kwa mashabiki wa klabu ya Man City, baada ya kuwa kinara wa upachikaji wa mabao katika msimu wa 2012-13.

Katika msimu huo ambao ilikuwa mara ya kwanza kwa Dzeko kucheza ligi ya Uingereza, akiwa na Man City baada ya kusajiliwa akitokea Wolfsburg nchini Ujerumani alifanikiwa kufunga mabao 15 na katika michuano yote aliyocheza alifunga jumla ya mabao 26.

Kuondoka kwa Dzeko, kunaacha maswali mengi kwa mashabiki wa klabu ya Man City, kutokana na mchezo wa ufunguzi wa ligi utakaowakabili mwanzoni mwa juma lijalo dhidi ya West Brom, kwani hadi wakati huu hakuna mshambuliaji wa kutumainiwa kikosini kwa kuwa Sergio Aguero kuwa majeruhi.

Meneja wa Man City ameshindwa kufanya usajili wa mshambuliaji ambaye ataziba pengo la Dzeko, hali ambayo inaendelea kuzusha hofu kubwa kwa mashabiki.

Chenge Akiri Kupokea Fedha Za Escrow, Apangua Gia Ya Sakata La IPTL
Mgosi Bosi Mpya Msimbazi