Shirikisho la Misri (EFA) limefanya marekebisho mapya manane kwa kanuni zao, pamoja na mabadiliko ya wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kwenye Ligi Kuu ya Misri.
Bodi ya EFA ilikutana Jumatatu (Jana) asubuhi pamoja na wawakilishi kutoka kila timu ya Ligi Kuu ya Misri. Shirikisho la soka la Misri lilitangaza maamuzi manane yafuatayo kufuatia kikao hicho:
1. FA Egyptian ya Misri imetangaza kuwa timu zitaruhusiwa kusajili makipa wa kigeni kuanzia msimu ujao. Ikumbukwe kuwa, Kanuni za mpira wa miguu za Misri zilikataza timu kusaini walinda mlango wowote wa kigeni katika kipindi cha miaka 12 iliyopita.
2. Ni wachezaji watano tu wa kigeni watakaoruhusiwa kwa kila timu, bila kujali nafasi.
3. Kipindi cha usajili wa msimu wa baridi kitakuwa tu Januari.
4. Timu za vijana zitashiriki katika mgawanyiko sawa na timu zao za wakubwa
5. Vilabu vimeomba utekelezaji wa mfumo mpya badala ya kutumia VAR, kwani inamakosa.
Hayo ni baadhi tu ya hayo 8:
Rais wa EFA, Ahmed Megahed, alisema kuwa ana mpango wa kumaliza ligi katikati ya Julai. Lakini kwa sababu ya uwepo wa magari 4 tu ambayo husafirisha mfumo wa VAR, kila wiki ya mchezo lazima ichezwe kwa siku zote tatu.